JAMHURI YA MUUNGANO TANZANIA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII

TANGAZO

Katibu Mkuu, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii anapenda kuwatangazia

Wauuguzi wa ngazi ya Astashahada na ngazi ya Stashahada

waliohitimu mafunzo mwaka 2013 wawasilishe maombi ya kupangiwa vituo vya kazi. Waombaji wanatakiwa kupendekeza maeneo matatu wanayotaka wapangiwe kazi.

Maeneo yenye nafasi za kazi yameainishwa kwenye tangazo la kazi

kwenye tovuti ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii

(www.moh.go.tz).

Maombi wayawasilishwe kwa

Katibu Mkuu,

Wizara ya Afya na Ustawi waJamii

 kwa anuani ya hapa chini kabla ya tarehe 14 Machi, 2014

Katibu Mkuu,

Wizara ya Afya na Ustawi

wa Jamii,

S.L.P. 9083,

DAR ES SALAAM

Share this


0 Comments